Haki na Majukumu
Inchini Marekani, sheria inalinda haki ya batu bote. Lazima ujifunze na kufuata sheria. Lazima ujue nini kinaweza kutokea ikiwa utavunja sheria. Kwenda kinyume na sheria kunaweza kusababisha kulipishwa faini au kufungwa jela na kuharibu hali yako ya uwamiaji. Unaweza hata kufukuzwa mu inchi.
Chagua muundo wa jinsi ambavyo ungependa kupata kwenye ukurasa huu. Unaweza kutazama video, kupakua hati ya maelezo au kusikiliza podikasti. Kila chaguo linatoa maelezo sawa.
Haki nne za msingi za kukumbuka:
- Una haki ya kiraia, kama vile uhuru wa kusema na kujiunga na dini yoyote.
- Una haki ya kufanya kazi. Hakuna mtu anayeweza kutumia rangi, dini, jinsia na asili ya kitaifa kukunyima kazi.
- Batoto bote bako chini ya umri wa miaka 18 bana haki ya kuwa salama na kulindwa dhidi ya madhara.
- Ikiwa wewe ni mhasiriwa wa uharifu, una haki ya kuchukuwa hatua ya kisheria. Ili kuripoti uharifu, ongeya na polisi. Ikiwa ni ya dharura, piga 911.
Majukumu manne ya muhimu ya kufuata:
- Ni kinyume cha sheria kumdhuru au kumuumiza mtu mwingine, wakiwemo watu wanafamilia. Madhara inahusu vitu kama, uonevu unyanyasaji, dhuluma/ya kijinsia, na unyanyasaji wa nyumbani.
- Ni kinyume cha sheria kumlazimisha mtu kutenda kinyume na idhini yake hapendi. Hakuna mtu anayeweza kukulazimisha kuolewa au kukulazimisha kufanya kazi na usilipwe.
- Ni kinyume cha sheria kuwanyanyasa watoto au kuwaacha watoto bila uangalizi wa mtu mzima.
- Ni kinyume cha sheria kununua, kuuzisha au kutumia dawa ya kulevya fulani, kama vile heroini na kokeini.
Sheria zingine mbili muhimu kujua:
- Lazima uwe na umri wa miaka 21 ili uruhusiwe kununua au kunywa pombe.
- Lazima uwe na lesensi ya dereva ili kuendesha gari.
Ready to test your knowledge?
Pakua programu ya Settle In
Get unlimited access to hundreds of lessons designed for all learners
Test your Knowledge
With short videos and interactive lessons, you can learn about a wide range of pre- and post-arrival resettlement topics like traveling to the U.S., housing, and looking for a job.