Language:

Kurekebisha Mila

Kurekebisha mila ni mwendo unaochukuwa muda mrefu. Mwendo huu ni tafauti kwa watu tofauti, lakini kuna hatua fulani katika huu mwendo ambazo watu wengi wana pitiya kwa Kurekebishwa kwa mila mpya. Pata maelezo zaidi kuhusu Marekebisho ya Kitamaduni nchini Marekani hapa chini.
22_2018.07.04_Charlottesville_AOberstadt_Grandpa1

Kurekebisha Mila

Kama wale wengine walioacha nyumba zao na kushimikwa kwa nchi ngeni, pengine utahisi wasiwasi na hasira unapojaribu kuzoweya nchi yako ngeni. Hisia hizi ni za kawaida na zina kuwa kwa muda. Unaweza hitaji miaka 2-5 ili uzoweye kabisa maisha ya shirika lako nyipya. Kuzoweya yako  itakuwa ya rahisi ikiwa utashirikiana na wale ambao wanakusaidia. Kuwa mtulivu, kuwa wazi na kujifunza njia nzuri za kushindana na shida na vikwazo vya mila inaweza kukusaidia kupunguza mwendo huu. Kupata kazi na kujifunza Kiingereza itakusaidia pia kuzoweya. Kujifunza kuishi katika mila mpya si rahisi, lakini inaweza kuwa pia zowezi nzuri wakati unajifunza mambo mapya na kupata ujuzi mpya.
CORE_Cultural Adjustment
20191102_AOberstadt_Boise_102

Mviringo wa U wa marekebisho ya mila

Kuna vipindi ine za kawaida za marekebisho ya mila ambazo unaweza kuta katika mwendo wako wa marekebisho: mwezi wa asali, kugongana kwa mila, marekebisho, na ujuzi. Awamu ya Honeymoon   Unakuwa na hisiya za msisimko na furaha, kila kitu ni kipya na cha kusisimua na ni kizuri. Iyi ina tokeya mara nyingi kisha ya kuwasili mahali mpya. Awamu ya Mshtuko wa Utamaduni Unakuwa na hisia za wasiwasi na kuchanganyikiwa kama vile mgeni,  jaribu kufanya kazi mahali ambapo ni tofauti na usipo pazoweya. Kipindi cha marekebisho Hisia zako zina punguka wakati una toka kwa kwa kipindi cha kugongana kwa mila na kuanza kujisikia vizuri zaidi na mjasiri katika shirika lako mpya. Awamu ya Umahiri Unakuwa na hisia ya faraja na maisha yako mapya na mila, hata ikiwa kuna kuwa nyakati zigumu pengine. Njia za kukabiliana na mgogangano wa mila zinaweza husisha kushirikiana na marafiki, kucheza michezo au kuwasiliana na vipato vya dini na vya kiroho. Ikiwa wewe au mwanameba wa jamaa yako anahisi kuwa hawezi kukakabiliana na matatizo ya maisha yako mapya Marekani, tafuta msaada mara moja. Kujihusisha na shirika za mahali kwa kuhuzuria matukio yaki mila au kujitolea pia kunaweza kusaidia kupunguza kuzoweya kwako maisha ya Marekani. Kushiriki kwa shirika ni njia ya kukutana na washiriki wengine wa kikundi chako cha kidini, lakini pia kukutana na Waamerika na kufanya mazoezi ya Kingereza. Wafanyakazi wa ushimikaji watakusaidia kujifunza mengi kuhusu shirika yako mpya. Chunguza shirika lako mwenyewe pia.
20201023_AOberstadt_NYC_46
Nguvu ya jamaa Ushimikaji inaweza tuma nguvu ya jamaa kwa kubadilisha majukumu yaliyopo. Mabadiliko katika majukumu ya jamaa ni moja katika sehemu zenye kusumbua ushimikaji ya wakimbizi. Hata hivyo, kuna njia nzuri za kukabiliana na mabadiliko haya ya majukumu. Kuwasiliana waziwazi na kwa uaminifu na wanamemba wa jamaa ili kila mtu awe na wazo nzuri la kile kila mtu katika jamaa anahisi na anachopitia. Wazazi wa wakimbizi wanaweza kabiliana na changamoto wakati watoto wao wanapo zoweya mila mpya kwa haraka na tofauti kuliko wao. Wazazi hawapendi mambo ambayo watoto wao wanataka kufanya au  njia nyingi wanazo zi zungumza na kutenda. Lakini zowezi fulani za uzazi zinaweza kuwa hazikubaliki au hata kinyume  ya sheria Marekani. Ikiwa una wasiwasi juu ya jamaa yako au unajitahidi na watoto wako, wasiliana na mtu katika Agence ya Réinstallation. Wanaweza kukusaidia au kukuunganisha na huduma za jamaa au mpango katika shirika lako. Maadili ya Marekani na kanuni za zaki mila Marekani ni jamii tofauti, undwa na watu wa jamii tofauti, ukabila, maoni ya kidini na zowezi nyingine au imani, bado kuna kanuni na matarajio ya kimila ambayo yanaenea kabisa Marekani. Kuonyesha uvumilivu na heshima kwa watu wote bila ingawa imani na asili zao ni thamani muhimu kwa Waamerika wengi. Unatakiwa kuwa na uvumilivu na heshima kwa wale walio tofauti na wewe na unapaswa kutarajia uvumilivu sawa na heshima kutoka kwa wengine. Zowezi zako fulani yaki mila yanaweza kutofautiana na ya Waamerika wengi. Zowezi nyingine zinaweza kuchukuliwa kuwa hayakubaliki na pengine kinyume na sheriya. Ingawa Waamerika wana uwazi kwa mila zao na njia za kufanya mambo, kuna maadili fulani ya msingi, imani na zowezi ambazo wanatarajia wakazi wa Marekani kufuata:
  • Filosofiya ya kuji tosheleza ki binafsi na utetezi wa kibinafsi ni muhimu kwa mila ya Marekani na kurekebisha mila.
  • Wamarekani wanaamini usawa wa jinsia na wanasamini uhuru wa wanaume na wanawake.
  • Watu wanatarajiwa kufika kwa wakati kwa ajili ya mpango waku kutanana na mikutano, ikiwa ni ya utaalamu au binafsi. Kuchelewa inaonekana kama kukosa heshima na kwa wakati mwingine kuchelewa kunaweza kuwa na matokeyo makubwa. Unaweza kupoteza kazi yako ikiwa unachelewa kufika kazini, na unaweza kupoteza mpango wakuku kutanana wako ikiwa hautakutana na mfanyakazi wako wa kesi kwa wakati, daktari au watoa huduma wengine.

Ready to test your knowledge?

Download the Settle In App

Get unlimited access to hundreds of lessons designed for all learners

Test your Knowledge

With short videos and interactive lessons, you can learn about a wide range of pre- and post-arrival resettlement topics like traveling to the U.S., housing, and looking for a job.
SettleIn Logo
Learn on the go
Maudhui kwenye tovuti hii yametengenezwa na Soko la Nyenzo za Mwelekeo wa Utamaduni (CORE), yako katika kikoa cha umma, na huenda ikatolewa tena. Yaliyomo kwenye tovuti hii yalitayarishwa chini ya makubaliano yaliyofadhiliwa na Ofisi ya Idadi ya Watu, Wakimbizi na Uhamiaji, Idara ya Jimbo la Marekani, lakini si lazima kuwakilisha sera ya wakala huyo na haipaswi kuidhinishwa na Serikali ya Shirikisho.