Haki na Majukumu

Tengenezeshwa:9/19/2024
Inchini Marekani, sheria inalinda haki ya batu bote. Lazima ujifunze na kufuata sheria. Lazima ujue nini kinaweza kutokea ikiwa utavunja sheria. Kwenda kinyume na sheria kunaweza kusababisha kulipishwa faini au kufungwa jela na kuharibu hali yako ya uwamiaji. Unaweza hata kufukuzwa mu inchi.

Haki nne za msingi za kukumbuka:

  1. Una haki ya kiraia, kama vile uhuru wa kusema na kujiunga na dini yoyote.
  2. Una haki ya kufanya kazi. Hakuna mtu anayeweza kutumia rangi, dini, jinsia na asili ya kitaifa kukunyima kazi.
  3. Batoto bote bako chini ya umri wa miaka 18 bana haki ya kuwa salama na kulindwa dhidi ya madhara.
  4. Ikiwa wewe ni mhasiriwa wa uharifu, una haki ya kuchukuwa hatua ya kisheria. Ili kuripoti uharifu, ongeya na polisi. Ikiwa ni ya dharura, piga 911.
Image
A wooden gavel resting on its sound block, symbolizing authority and justice. The gavel is polished and placed on a wooden surface.
Image
An empty courtroom featuring wooden furnishings, a judge's bench, jury seats, and a witness stand. The room is well-lit with chandeliers hanging from the ceiling, and an American flag is visible behind the judge's bench.

Majukumu manne ya muhimu ya kufuata:

  1. Ni kinyume cha sheria kumdhuru au kumuumiza mtu mwingine, wakiwemo watu wanafamilia. Madhara inahusu vitu kama, uonevu unyanyasaji, dhuluma/ya kijinsia, na unyanyasaji wa nyumbani.
  2. Ni kinyume cha sheria kumlazimisha mtu kutenda kinyume na idhini yake hapendi. Hakuna mtu anayeweza kukulazimisha kuolewa au kukulazimisha kufanya kazi na usilipwe.
  3. Ni kinyume cha sheria kuwanyanyasa watoto au kuwaacha watoto bila uangalizi wa mtu mzima.
  4. Ni kinyume cha sheria kununua, kuuzisha au kutumia dawa ya kulevya fulani, kama vile heroini na kokeini.
Image
A view of the United States Supreme Court building, featuring its grand neoclassical architecture with tall columns and a detailed pediment. An American flag is flying in front of the building, and the scene is set against a clear blue sky.

Sheria zingine mbili muhimu kujua:

  1. Lazima uwe na umri wa miaka 21 ili uruhusiwe kununua au kunywa pombe.
  2. Lazima uwe na lesensi ya dereva ili kuendesha gari.

Pia lazima ujifunze kuhusu sheria za serikali kuu na serikali za mitaa. Hii inajumuisha sheria zinazohusiana na uvutaji sigara katika maeneo ya umma, makazi, na uvuvi na uwindaji bila leseni.

Kumbuka: Kuna sheria nyingi nchini Marekani. Kutokujua sheria hakuzuii kuadhibiwa ukivunja sheria.

Image
Screenshot of Settle In app
Image
App Icon

Jaza programu ya Settle In

Tazama video fupi, masomo ya kutendana, na beji ya kufuata maendeleo yako ya kujifunza Settle In ndiyo mwenzako msaidizi katika safari yako ya kutafuta makao mupya

Was this article helpful?
0
0