Jinsi ya Kushirikiana na Polisi nchini Marekani
Tengenezeshwa:11/18/2024
Jukumu la polisi nchini Marekani ni kudumisha utulivu na usalama wa umma, kutekeleza sheria, na kulinda haki za raia za watu binafsi jamii zilizo kote nchini. Jifunze Zaidi hapo chini.
Iwapo una dharura, unaweza kuhitaji kupiga simu kwa 9-1-1 ili kuomba usaidizi. Kama vile wazima moto na huduma za ambulansi, polisi wanaweza kufika ili kukusaidia. Unaweza pia kukutana na polisi katika hali mbalimbali katika jamii zenu kama vile wanapowasimamisha madereva kwa kutofuata sheria za barabara.
Ikiwa utakutana na polisi katika maeneo ya umma, wakusimamishe wakati unaendesha gari au kukabiliana nao katika mazingira yoyote, hivi hapa ni baadhi ya vidokezo vya njia zinazofaa za kushirikiana nao:
- Usiwe na wasiwasi na udhibiti hisia zako.
- Kuwa mwenye heshima. Usibishane.
- Weka mikono yako ikiwa inaonekana na nje ya mifuko yako.
- Usikimbiye au kuchukua kitu chochote kwa ghafla.
- Kaa mahali pamoja na uwe mtulivu.
- Ikiwa uko kwenye gari, kaa ndani ya gari na ufunge mshipi wa usalama.
- Usimguse au kusimama karibu sana na ofisa wa polisi.
- Tembea na kitambulisho chako na uwe na nambari ya simu ya mtu anayeweza kukusaidia, ikihitajika.
- Uliza ikiwa uko huru kuondoka na ikiwa ni hivyo, ondoka kwa utulivu.
Image
Image
Kumbuka: Ni sawa kusema kuwa hauelewi. Una haki ya kisheria ya kupewa huduma ya mkalimani.
- Ikiwa utashutumiwa kwa kuvunja sheria na ukamatwe, una haki ya kukaa kimya na kuzungumza na wakili kabla ya kuhojiwa.
- Ikiwa huwezi kugharamia huduma za wakili, mahakama itakulipia gharama za wakili atakayekuwakilisha.
- Ikiwa una maswali kuhusu jinsi ya kushirikiana na polisi, hakikisha kuwa umeuliza wafanyakazi walio katika ofisi iliyokupa makazi ili upate usaidizi.
Image