Jukumu la Watu nchini Marekani walio na uhusiano na wahamiaji katika Utoaji wa Makazi kwa Wakimbizi

Tengenezeshwa:10/29/2024
Wakimbizi wanaokuja Marekani kupitia Mpango wa Uandikishaji wa Wakimbizi Nchini Marekani (USRAP) wana fursa ya kutambua mtu nchini Marekani aliye na uhusiano na mhamiaji kupitia Kituo cha Uombaji wa Usaidizi kwa Wakimbizi cha Kupelekwa Kuishi Marekani ambacho kinasaidia katika kushughulikia kesi yao. Tofauti na mwanafamilia rasmi anayeandikisha Hati ya Kiapo cha Uhusiano, ombi la I-730 au wakati mwingine ombi lililoidhinishwa la I-130, wakimbizi wanaweza kuchagua kutambulisha mtu yeyote, bila kujali uhusiano wao, kama mtu nchini Marekani aliye na uhusiano na mhamiaji ambaye wangependa kuishi karibu naye. Hakuna masharti kwa wakimbizi kutambulisha watu wowote wanaoishi Marekani walio na uhusiano na wahamiaji wakati kesi yao inaposhughulikiwa nje ya nchi. Hata hivyo, ikiwa mtu huyu atatambulishwa, ni muhimu kwa wakimbizi na watu wanaoishi Marekani walio na uhusiano na wahamiaji kuelewa jukumu la mtu anayeishi Marekani aliye na uhusiano na mhamiaji katika utoaji wa makazi kwa wakimbizi nchini Marekani. Jifunze Zaidi hapo chini.
Image
Refugee Resettlement

Mtu Anayeishi Marekani aliye na uhusiano na mhamiaji ni nani?

Wakimbizi wanaopata makazi mapya nchini Marekani wanaweza kutambua marafiki au jamaa ambao tayari wanaishi Marekani na ambao wangependa kuunganishwa tena nao baada ya kuwasili. Baada ya kutambulishwa, Makazi Mapya litawasiliana na watu hao ili kuthibitisha ikiwa wangependa wakimbizi wapewe makazi mapya karibu nao. Wakikubali, watu hawa watachukuliwa kama watu wanaoishi Marekani walio na uhusiano na wahamiaji. Shirika la Makazi Mapya halitashiriki maelezo ya kibinafsi ya wakimbizi, kama vile maelezo ya kiafya na anayeishi Marekani aliye na uhusiano na mhamiaji. Hata hivyo, litashirikiana na mtu anayeishi Marekani aliye na uhusiano na mhamiaji ili kuweka matayarisho ya kuwapokea wakimbizi wanaowasili Marekani. Watu wanaoishi Marekani walio na uhusiano na wahamiaji hawawajibiki kifedha au kisheria kwa jamaa au marafiki wao ambao ni wakimbizi wapya wanaowasili Marekani. Hata hivyo, wanaweza kutekeleza jukumu muhimu katika shughuli ya wakimbizi kupata makazi mapya kwa kutoa usaidizi katika hali ya kupata makazi mapya kwa marafiki au jamaa zao kwa kushirikiana na Shirika la Makazi Mapya. Ni muhimu kukumbuka kuwa lengo la wakimbizi, kwa usaidizi wa Shirika la Makazi Mapya, ni kuweza kujitegemea kiuchumi kupitia kuajiriwa haraka iwezekanavyo baada ya kuwasili Marekani.

Image
Resettlement
Image
Three people are standing together in a room, closely looking at a piece of paper. A man in a white jacket, a woman with blonde hair in a gray sweater, and a boy in a black and green jacket are intently reading the document. The setting appears to be a casual indoor environment.

Shirika la Makazi Mapya ni nini?

Shirika la Makazi Mapya ni shirika lisilo la faida ambalo hushirikiana na Serikali ya Marekani katika mpango wa ushirikiano kati ya mashirika binafsi na umma ili kuwasaidia wakimbizi wanaokuja Marekani kupitia USRAP. Serikali ya Marekani huweka mwongozo na kutoa ufadhili usio kamili kwa huduma za msingi zinazohitajika ambazo wakimbizi hupokea kupitia Mapokezi na mpango wa Uwekaji (R&P). Mashirika ya Makazi Mapya yanawajibika kwa kutoa huduma hizi na hutoa usaidizi muhimu zaidi kwa wakimbizi na familia zao katika miezi yao ya kwanza nchini Marekani. Ili upate maelezo zaidi kuhusu Shirika la Makazi Mapya, tembelea tovuti ya Settle In website katika https://settleinus.org.

Image
A man and a woman, both wearing blue polo shirts with the restaurant's name, are standing inside a restaurant. The woman has her arms crossed, and the man has his arm around her shoulder. Behind them is the counter with a menu board above, displaying various food items. The kitchen area and some framed pictures on the wall are also visible.

Watu Wanaoishi Marekani walio na Uhusiano na Wahamiaji Hushirikiana Vipi na Shirika la Utoaji wa Makazi Mapya?

Shirika la Makazi Mapya litawasiliana na mtu anayeishi Marekani aliye na uhusiano na mhamiaji kwa mara ya pili wakati wa kuwasili kwa marafiki au jamaa utakapokuwa umekaribia ili kufafanua mpango wa R&P na huduma za msingi zinazohitajika. Mawasiliano haya ya pili yanaweza kutokea baada ya miezi au miaka kadhaa baada ya mawasiliano ya kwanza na mabadiliko yoyote ya anwani ya mawasiliano ya mtu anayeishi Marekani aliye na uhusiano na mhamiaji yanapaswa kuwasilishwa kwa Shirika la Makazi Mapya, ikiwa ni pamoja na iwapo mtu anayeishi Marekani aliye na uhusiano na mhamiaji amebadilisha anwani yake.

Shirika la Makazi Mapya linapowasiliana na mtu anayeishi Marekani aliye na uhusiano na mhamiaji wakati wa kuwasili kwa wakimbizi utakapokuwa umekaribia, litamwuliza mtu anayeishi Marekani aliye na uhusiano na mhamiaji ikiwa angependa kuhusishwa katika huduma na usaidizi wa utoaji wa makazi mapya kama vile kuambatana na Shirika la Makazi Mapya kuenda kuchukua marafiki au jamaa zake kwenye uwanja wa ndege, kutoa makao au usafiri wa kuhudhuria miadi au kuwaelekeza wakimbizi katika mazingira ya jamii yao mpya. Shirika la Makazi Mapya linawajibika kikamilifu kwa kutoa huduma hizi na kubainisha matumizi ya ufadhili wa R&P kwa wakimbizi. Usaidizi wowote unaotolewa na watu wanaoishi Marekani walio na uhusiano na wahamiaji ni wa kujitolea. Baadhi ya Mashirika ya Makazi Mapya yanaweza kuwa na “Makubaliano na Mtu Anayeishi Marekani aliye na Uhusiano na Mhamiaji” ambayo ni fomu ambapo Watu wanaoishi Marekani Walio na uhusiano na wahamiaji huonyesha usaidizi wanaoweza kutoa kwa rafiki au jamaa anapowasili Marekani. Fomu hii si hati ya kisheria lakini ni zana ya kusaidia watu wanaoishi Marekani walio na uhusiano na wahamiaji na wafanyakazi wa shirika.

 

Faida na Manufaa kwa Wakimbizi na Watu Wanaoishi Marekani walio na Uhusiano na Wahamiaji

Wakimbizi wanaweza kunufaika kutokana na usaidizi wa ziada unaotolewa na watu wanaoishi Marekani walio na Uhusiano na Wahamiaji kwa njia nyingi. Watu wanaoishi Marekani walio na uhusiano na wahamiaji wana fursa ya kipekee ya kushiriki hali zao za kibinafsi kuhusu maisha nchini Marekani na marafiki au jamaa zao ambao ni wakimbizi wapya wanaowasili wanapoingiliana na mifumo mipya na ya kigeni, pamoja na tofauti za kitamaduni. Ni muhimu pia kutambua kwamba hali ya kila mkimbizi nchini Marekani ni tofauti na inaweza kusababishwa na vigezo kama vile umri, eneo la makazi mapya, pamoja na kazi na ujuzi wa lugha.

 

Lugha na Ukalimani

Ingawa watu wanaoishi Marekani walio na uhusiano na wahamiaji huenda wanazungumza Kiingereza na lugha ya wakimbizi, wafanyakazi wa Shirika la Makazi Mapya hawawezi kutumia watu wanaoishi Marekani walio na uhusiano na wahamiaji kama wakalimani wanapowasiliana na wakimbizi. Serikali inahitaji Shirika la Makazi Mapya litumie mkalimani wa kujitegemea ikiwa hakuna mfanyakazi wao yeyote anayezungumza lugha ya mkimbizi. Wakati mwingine ambapo

Shirika la Mapya halitoi huduma ya msingi inayohitajika, marafiki wanaoishi Marekani wanaweza kuwafasiria marafiki au wanafamilia wao wapya waliowasili. Shirika linaweza kutoa mwongozo kuhusu ukalimani jinsi inavyohitajika. Watu wanaoishi Marekani walio na uhusiano na wahamiaji wanahimizwa kusisitiza umuhimu wa kujifunza Kiingereza na kushiriki katika mafunzo ya kujifunza Kiingereza katika jamii yao.

Je, Wajua?

Yafuatayo ni maelezo kuhusu utoaji wa makazi kwa wakimbizi nchini Marekani yanayohusiana zaidi na wakimbizi walio na watu wanaoishi Marekani walio na uhusiano na wahamiaji. Ili upate maelezo zaidi kuhusu USRAP na maisha nchini Marekani, tembelea tovuti ya CORE Resettlement Navigator katika corenav.org. Tovuti hii inatoa maelezo yanayoeleweka, sahihi na yaliyosasishwa kwa wakimbizi na wale wanaowasaidia katika kupata makazi mapya nchini Marekani.

Mwongozo uliowekwa na Serikali ya Marekani kwa USRAP unaweza kubadilika kila mwaka na hivyo basi kuathiri huduma na usaidizi unaotolewa na Mashirika ya Makazi Mapya kwa wakimbizi. Kwa hivyo, huduma za msingi za kupata makazi mapya zilizotolewa kwa wakimbizi wa zamani, ambao huenda baadaye wakawa watu wanaoishi Marekani walio na uhusiano na wahamiaji, zinaweza kuwa tofauti na huduma zinazotolewa kwa wakimbizi wapya wanaowasili..

Ni lazima Shirika la Makazi Mapya lirekodi kukamilishwa kutolewa kwa huduma za msingi zinazohitajika ikiwa ni pamoja na kuthibitisha huduma zozote zinazotolewa na watu wanaoishi Marekani walio na uhusiano na wahamiaji. Hii ndiyo sababu watu wanaoishi Marekani walio na uhusiano na wahamiaji wanaweza kuombwa kuweka saini kwenye hati inayohusiana na huduma wanazotoa. Hata hivyo, si lazima watu wanaoishi Marekani walio na uhusiano na wahamiaji watoe huduma zozote za msingi zinazohitajika.

Mara nyingi, watu wanaoishi Marekani walio na uhusiano na wahamiaji hufurahia kuhusishwa katika kusaidia kutoa makazi mapya kwa marafiki na jamaa zao ambao ni wakimbizi wapya wanaowasili, iwe ni kuwakaribisha kuishi nao nyumbani kwao, kuwapeleka kuhudhuria miadi au kutoa tu usaidizi wa kihisia na kijamii. Ikiwa watu wanaoishi Marekani walio na uhusiano na wahamiaji wanaripoti saa wanazotumia kutoa huduma za kujitolea kwa Shirika la Makazi Mapya, wanapaswa kuthibitisha na wafanyakazi wa Shirika la Makazi Mapya ili kuona shughuli ambazo zinaweza kuhesabiwa kama usaidizi wa kujitolea.

Image
A smiling woman wearing a black hat is holding a baby and standing in a group with other women. The baby is looking curiously at one of the women in the group. The setting appears to be casual and friendly.
Je, makala hii ilikusaidia?
14
0