Huduma za Makazi Mapya

Tengenezeshwa:10/30/2024
Wakala wa Kutafuta Makazi Mapya ni shirika lisilo la faida linaloshirikiana na Serikali ya Marekani katika ushirikiano wa umma na mashirika binafsi ili kuwasaidia wakimbizi wanaokuja Marekani kupitia Mpango wa Uhamiaji wa Wakimbizi wa Marekani. Pata maelezo zaidi kuhusu Wakala wako wa Makazi mapya hapa chini.

Kuna Wakala tisa za Kutafuta Makazi nchini Marekani ambazo hufanya kazi katika ngazi ya kitaifa. Wakala hizi za kitaifa za Kutafuta Makazi zina ofisi za eneo katika miji ambapo wakimbizi wanaishi, ingawa ofisi hizi za eneo zinaweza kuhudumu chini ya majina tofauti.

Baadhi ya Wakala za Kutafuta Makazi zina mweleko wa kidini, lakini haziruhusiwi kubagua wakimbizi kwa misingi ya rangi, asili, taifa au jinsia, au kwa misingi ya ulemavu wa kimwili au wa akili.

Wakala hizi za Kutafuta Makazi zimekuwa zikiwasaidia wakimbizi kutoka duniani kote kuanza kuishi Marekani kwa miaka mingi. Zinatoa usaidizi muhimu kwa wakimbizi na familia zao katika miezi yao ya kwanza nchini Marekani.

Image
Resettlement Services
Image
Resettlement Services

Jukumu la Wakala za Kutafuta Makazi

Serikali ya Marekani inaweka miongozo na kufadhili huduma za msingi ambazo wakimbizi hupata, lakini Wakala za Kutafuta Makazi na mashirika mengine hutoa huduma na zinaweza kutoa usaidizi mwingine pia. Wakala wa Kutafuta Makazi itakuunganisha na huduma nyingine ambazo unahitaji ili uanze maisha yako mapya. Huduma na usaidizi ni wa kiasi kidogo, na wakimbizi tofauti wanaweza kupokea huduma tofauti kwa sababu ya mambo kama vile ukubwa wa familia, umri wa wanafamilia, mahali wamepewa makazi mapya, na mapato.

Siku 30 za Kwanza

Huduma za kwanza hunuiwa kuwasaidia wakimbizi kuanza maisha mapya nchini Marekani. Wakala za Kutafuta Makazi zitakusaidia kwa huduma za msingi na gharama za kuishi katika siku zako 30 za kwanza nchini Marekani. Baadhi ya wakala zitalipia gharama zako moja kwa moja. Nyingine zinaweza kukupa baadhi ya fedha na kukuonyesha jinsi na mahali pa kulipia gharama fulani.

Hadi Siku 90

Kipindi cha siku 30 kinaweza kuongezwa hadi siku 90 baada ya kuwasili kama huduma za kupata makazi mapya unazohitaji haziwezi kukamilishwa kwa siku 30. Utahitaji kuanza kutafuta ajira haraka iwezekanavyo. Wakala ya Kutafuta Makazi haihitajiki kukutafutia ajira. Wakala wa Kutafuta Makazi pia haihitajiki kukupa simu, televisheni, gari, au kompyuta, au kukulipia mkopo wa usafiri na bili nyingine. Utahitaji kufanya kazi ili upate fedha za kununua vitu hivi na kulipia gharama zako mwenyewe.

Kuhamia kwenye Jamii Nyingine

Kuna sababu nyingi nzuri za kukaa katika jamii ulipotafutiwa makazi kwa angalau miezi sita hadi mwaka mmoja. Ikiwa unataka kuhamia kwenye jamii nyingine, utawajibikia kuhama kwako na kutafuta huduma zozote za usaidizi ambazo unaweza kuhitaji katika jamii  yako mpya Ni vyema kujadili na Wakala wa Kutafuta Makazi kuhusu nia yako ya kuhama kabla ya kuondoka Lazima uijulishe Serikali ya Marekani anwani yako mpya ndani ya siku kumi baada ya kuhama.

Huduma Zinazohitajika

Hizi ndizo huduma ambazo wakala zote za kutafuta makazi lazima ziwape wakimbizi wote au kuhakikisha kwamba kuna mtu ambaye anazitoa katika siku zao 30 kwanza nchini Marekani:

  • Kukutana na wakimbizi kwenye uwanja wa ndege na kutoa usafiri kwenda nyumbani.
  • Kutoa mavazi muhimu yanayofaa kwa kila msimu. Sio lazima mavazi yawe mapya, lakini yanapaswa kuwa safi na ya hali nzuri.
  • Kupangia nyumba salama, safi na ya hali nzuri.
  • Kumpa kila mtu mzima katika familia kiasi kidogo cha fedha za matumizi ya kibinafsi.
  • Kuleta samani za kimsingi na vifaa vya nyumbani. Sio lazima vifaa hivi viwe vipya, lakini vinapaswa kuwa safi na vya hali nzuri.
  • Kutoa chakula au marupurupu ya chakula kulingana na ukubwa wa familia hadi familia hii ipokee msaada wa chakula cha serikali au iweze kujitafutia chakula.
  • Kusaidia kuwasilisha ombi la fedha na usaidizi wa kimatibabu.
  • Kusaidia kuwasilisha ombi la kupewa kadi ya Usalama wa Jamii.
  • Kusaidia kujiandikisha katika elimu ya lugha ya Kiingereza, ikihitajika.
  • Kutoa usafiri kwenda mahojiano ya kazi na mafunzo ya kazi.
  • Kusaidia kujiandikisha katika huduma za ajira, ikihitajika.
  • Kusaidia kufanyiwa uchunguzi wa afya na huduma zozote za afya zinazohitajika.
  • Kusaidia kujiandikisha katika Huduma Maalum kwa wanaume wa umri wa kati ya miaka 18 na 25.
  • Kusaidia kuwaandikisha na kuwasajili watoto shuleni.
  • Kutoa mwongozo wa kijamii na maisha nchini Marekani.
  • Kutoa usafiri na tafsiri, ikihitajika, kwa huduma zote zinazohitajika.
Image
Screenshot of Settle In app
Image
App Icon

Jaza programu ya Settle In

Tazama video fupi, masomo ya kutendana, na beji ya kufuata maendeleo yako ya kujifunza Settle In ndiyo mwenzako msaidizi katika safari yako ya kutafuta makao mupya

Je, makala hii ilikusaidia?
32
-2