Mapitio ya Mpangilio wa Programme ya Réception na Placement (R&P) ya Marekani.

Tengenezeshwa:10/16/2024
Ukifika mwisho wa marudio yako Marekani, mwakilishi wa ofisi ya Réinstallation (au jamaa wako anayeishi Marekani, kama unaye) atakulaki katika uwanja wa ndege kukukaribisha. Utasafirishwa mpaka mahali salama na nyumba iliyotengwa kwa ajili yako na familia yako. Jifunze Zaidi hapo chini.

Mapito ya Réception na Placement

Nyumba hio itakuwa na samani za msingi, vyombo vya nyumba na ugavi wa awali wa chakula. Muda mfupi baada ya kuwasili, utakutanana wafanyakazi wa Agence ya Réinstallation. Ofisi ya Agence ya Réinstallation itawapa Programme ya Réception na Placement (R&P)  huduma na kukuunganisha na huduma zingine za kijamii wakati wa siku zako za kwanza 30 hadi 90 nchini Marekani. Mfanyikazi wa ofisi ya Réinstallation yuko huko kukusaidia na atakuwa nguzo yako msingi ya mawasiliano. Wafanyikazi hao watashughulikia maslahi yako ya haraka.

Usijali kama huwezi kuwasiliana kwa Kiingereza kwa maana huduma zote za utafsiri zinazohitajika zitatolewa inavyohitajika. Kila mtu mzima katika familia yako atapewa pesa kidogo kwa matumizi yake ya kibinafsi. Pia utapewa chakula au posho ya chakula kulingana na ukubwa wa family yako. Wafanyakazi watakusaidia kuomba Kadi ya Sécurité sociale, ambayo ni muhimu kupata ajira na faida zingine nchini Marekani.

Watakusaidia kujisajilisha katika huduma za ajira ambazo zitakusaidia katika shughuli zako za kutafuta kazi. Kutafuta, kupata na kuhifadhi kazi itakuwa muhimu kwa maisha ya badaye na kujikimu kwa familia yako. Kuajiriwa ni njia ya haraka zaidi ya Auto suffisance na inayohitajika kwa mafanikio. Mafunzo ya shule kwa watoto wote ni lazima Marekani. Utasaidiwa kusajili watoto wako katika shule ya umma, ambayo ni bure. Iwapo wewe na familia yako hamzungumzi Kiingereza, wafanyakazi wa ofisi ya Réinstallation watawasaidia na kuwasajilisha katika Darasa la mafunzo ya lugha ya Kiingereza.

Watakusaidia wewe na familia yako kupata hatua ya  mwanzo ya Uchunguzi wa Matibabu na watakueleza kuhusu jinsi unavyoweza kupata na kulipia huduma za kiafya unapozihitaji. Watakusaidia pia kupata Assurance ya Matibabu kama iwapo muajiri wako hapeani, au bima ya kiserikali ya afya kama umehitimu.

Ofisi ya Réinstallation itatoa Orientation Culturelle ambayo itazingatia Orientation Culturelle uliohudhuria kutoka Centre de Support pour la Réinstallation. Orientation Culturelle utakusaidia kujifunza kuhusu jamii yako ngeni. Kutoka wakati unapowasili Marekani, unalindwa na sheria sawa zinazolinda wakazi wote wa Marekani.

Utajifunza kuhusu haki na majukumu yako kama mkazi wa kisheria na jinsi ya kupata usaidizi unapouhitaji. Katika siku za mwanzo 30 hadi 90 za kipindi cha Programme ya Réception na Placement (R&P) , wafanyikazi wa Réinstallation watafanya kazi pamoja na wewe ili kutengeneza na kutekeleza mpango wa kukusaidia kuwa Auto Suffisant. Ikiwa usaidizi wa ziada unahitajika zaidi ya zile siku 30 hadi 90, watakuunganisha na huduma zingine za kijamii au za kiserikali.

Image
Resettlement Placement
Image
Resettlement Placement
Image
Screenshot of Settle In app
Image
App Icon

Jaza programu ya Settle In

Tazama video fupi, masomo ya kutendana, na beji ya kufuata maendeleo yako ya kujifunza Settle In ndiyo mwenzako msaidizi katika safari yako ya kutafuta makao mupya

Je, makala hii ilikusaidia?
8
0