Ajira kwa Wanawake Wakimbizi

Tengenezeshwa:10/29/2024
Ajira nchini Marekani ni muhimu sana kwa maisha ya baadaye na ustawi wa familia yako, pamoja na maendeleo yako mwenyewe na utulivu wa kifedha kama mwanamke. Watu wote wazima, wanawake na wanaume, walio kati ya umri wa miaka 18 na 64 na wanaoweza kufanya kazi, wanapaswa kuupa kipaumbele utafutaji kazi. Jifunze Zaidi hapo chini.

Manufaa ya Kufanya Kazi

Nchini Marekani, idadi ya wanawake ni nusu ya wafanyakazi, hufanya kazi sawa na wanaume katika viwango vyote, na mara nyingi huwasimamia wafanyakazi wa kiume. Kupata na kudumisha kazi kuna faida nyingi kwako wewe na familia yako.

Kuisadia familia kumudu mahitaji – Wakati wanandoa wote wawili wanafanya kazi, mapato ya familia huongezeka, hivyo kuwa rahisi kumudu gharama kama vile matumizi ya kila mwezi na kulipia kodi ya nyumba, na pia chakula na nguo. Mapato mara mbili pia inakuwezesha kuokoa pesa na kuongeza usalama wa kifedha wa familia.

Kupokea manufaa ya ajira – Baadhi ya kazi hujumuisha marupururpu maalum kama vile bima ya afya ambapo mwajiri humpa mfanyakazi mipango ya bima na mara nyingi hulipa sehemu ya gharama ya kila mwezi. Malipo yote ya bima hukatwa kwenye malipo ya mfanyakazi. Wamarekani wengi hutegemea mipango ya bima ya afya ya ajira kwa sababu  gharama ya huduma za afya ni kubwa na bima ya afya husaidia kupunguza gharama hizo. Kupokea bima ya afya kupitia mahali pa kazi yako ni manufaa makubwa.

uboresha Kiingereza chako – Kufanya kazi nje ya nyumbani kutakuwezesha kufanya mazoezi na kuboresha Kiingereza chako unaposhirikiana na wafanyakazi na wateja katika mazingira ya kitaaluma. Kujifunza Kiingereza itakuwezesha kushiriki katika jumuiya yako na kuongeza uwezo wako wa kusimamia mambo yako ikiwa unakwenda kwenye duka la vyakula, ofisi ya daktari, au benki.

Kushirikiana na wengine – Mahali pa ajira pia panakupa fursa ya kushirikiana na watu mbalimbali na kujifunza kuhusu utamaduni na maadili ya Marekani, ambayo yatakuwezesha kuzoea mazingira yako mapya. 

Kupata ujuzi wa kitaalamu – Kazi yako ya kwanza itakupa ujuzi na ustadi wa kitaalamu ambao utakuandaa kwa kazi zako za baadaye. Jinsi unavyopata ujuzi zaidi ndivyo unavyopata nafasi kubwa zaidi ya  kupandishwa cheo kazini au kupata kazi bora zaidi.

Kutumia usafiri wa umma au kujifunza kuendesha gari – Kusafiri kwenda  na kutoka kazini kunaweza kukuhitaji utumie usafiri wa umma au ujifunze kuendesha gari. Kujua jinsi ya kutumia usafiri wa umma au kuendesha gari kutachangia sana katika uhuru wako na kujitegemea, kukusaidia kujua mji wako na mahali unapoishi, na kukupa hisia ya kujumuika katika jamii yako mpya.

Image
Employment
Image
Employment

Kina Mama wafanyakazi na Kina Mama ambao hawajaolewa

Wanawake wengi ambao hulea watoto wadogo mara nyingi huwa na ugumu kugusa mahitaji ya kazi na nyumbani, hasa ikiwa ni mama wa pekee. Hata hivyo, kuna ufumbuzi wa kusaidia mama wanaofanya kazi nje ya nyumba. Suluhisho moja ni kuwapeleka watoto katika vituo vya utunzaji wa mchana. Huduma za utunzaji wa mchana hulipishwa. Early Head Start ni mpango uliofadhiliwa na serikali kuu inayowahudumia watoto wa familia za mapato ya chini kutoka kuzaliwa hadi umri wa miaka 3. Mpango mwingine, Head Start huzihudumia familia zilizo na watoto wa umri wa miaka 3 hadi 4. Kuandikisha watoto wadogo katika mojawapo ya mipango hii kutamwezesha mama ambaye hajaolewa, au wazazi wote wawili, kufanya kazi nje ya nyumbani. Suluhisho jingine ni kutumia marafiki, majirani au watu wazima wa familia kama vile babu na bibi kama walezi wa watoto kuwasaidia wazazi wanaofanya kazi. Kwa wanandoa, suluhisho la tatu ni kwa mmoja wa wazazi kutafuta kazi ya nusu siku ya saa za jioni na mwishoni mwa wiki, ambayo itamwezesha mzazi mmoja kuwalea watoto huku mzazi mwingine akiwa kazini.

Image
Employment

Hali za Familia Zinazobadilika

Wamarekani wanathamini uhuru katika wanaume na wanawake. Katika familia nyingi, mume na mke wote hufanya kazi, na katika familia nyingine, mke hupata malipo zaidi kuliko mume. Katika familia zingine, mke amepata kazi na mume hana. Katika hali hii, mume atatarajiwa kuwatunza watoto wakati hawako shuleni.

Katika hali kama hizo, wanaume wengine wanaweza kuhisi kwamba wamepoteza nafasi yao ya uongozi katika familia. Wanawake wengine wanaweza kuhisi dhiki wanapopata majukumu mapya na kuwa mfanyakazi mkuu wa familia. Kusaidiana, pamoja na mawasiliano ya wazi na ya uaminifu, inaweza kuongeza uelewano kupunguza matatizo kati ya wanandoa.

Image
Employment
Image
Employment
Image
Screenshot of Settle In app
Image
App Icon

Jaza programu ya Settle In

Tazama video fupi, masomo ya kutendana, na beji ya kufuata maendeleo yako ya kujifunza Settle In ndiyo mwenzako msaidizi katika safari yako ya kutafuta makao mupya

Je, makala hii ilikusaidia?
4
-1